Imeandaliwa na;
Charles Stephen Asande:
MJASILIAMALI
-Ni mtu anayetafuta fursa yenye manufaa na kuamua kuiweka katika biashara.
SABABU TOFAUTI ZINAZOWAPELEKA WATU KATIKA UJUASILIAMALI
-Kuchoshwa na Kazi za kuajiriwa
Hapa ni mahali mtu anaweza kupanga ratiba(biashara) zake bila kuingiliwa na nguvu yeyote(Shinikizo).
-Hitaji la kutatua mactatizo ya watu(kibiashara)
Uwepo wa matatizo katika jamii ndio unaopelekea wajasiliamali kuwepo.Hapa wao huona kwanza tatizo kisha hulitatua kwa njia zitazowainua wao wakati huohuo zikitatua tatiza husika katika jamii.
-Hitaji la kufanikiwa kimaisha
Wajasiliamali ni watu wanaojenga/kuimarisha uchumi hivo kupelekea maisha yao pia kuwa ya mafanikio.
-Kuondokana na tatizo la kukosa ajira
Kutokana na Mitikisiko ya kiuchumi makampuni mengi tena makubwa yamekuwa yakipunguza wafanyakazi kuliko wanaowaajiri.Hivyo iwe kwa msomi au mtu mwingine wa kawaida ni lazima kulifikiria hili jambo kwa umakini.Hapa ndipo watu huona njia inayowapelekea katika ujasiliamali.
-Hamu ya kutaka kuishi maisha uyapendayo
Kuanza biashara kunakufanya kuwa huru kupanga lini,wapi na namna gani ufanye shughuli zako
-Tabia za watu wenye maendeleo
1.MAONO MAKINI
Mjasiliamali huanza na wazo kuu lenye kubeba jinsi/namna gani anaweza kulifanya WAZO LAKE KIBIASHARA(Bussiness Idea) lifanikiwe
2.KUJITUMA
Mjasiliamali siku zote huwa tayari kufanya kazi tena kwa bidii ili kufikia malengo yake
3.UBUNIFU
Mjasiliamali hubuni mbinu rahisi kukabiliana na matatizo/hali ngumu kwa jamii/mazingira aliyopo
4.UTAYARI.
Mjasiliamali hana hofu katika gumu lolote analokutana nalo, Zaidizaidi yeye hujipanga vema na kuendelea mbele
5.UVUMILIVU
Katika kila unapopita kuna hali unaweza kutana nazo ambazo zinakuhitaji kuwa mvumilivu.Vivohivo kwa mjasiliamali kuna wakati unaweza ona hakuna dalili ya mafanikio kwa wakati ujao lakini usikate tamaa jibidishe zaidi na zaidi.Siku zote hakuna njia ambayo ni mteremko moja kwa moja.
6.NIDHAMU
Katika Maendeleo hiki kipengele ni muhimu.Unaweza ukawa na biashara nzuri lakini ukiwa na nidhamu mbovu unaweza kuta unapiga marktime(hauendelei).Kama mjasiliamali yapasa kuwa na nidhamu kwa biashara yako(wateja wako) na matumizi yako(Nidhamu ya pesa).
Ili kutunza nidhamu fanya yafuatayo:
-Ujue vitu vyote vinavyoshusha nidhamu katika nyanja zako zote kibiashara(n.b biashara na matumizi) Kwa mfano kuchat,kucheza bao,drafti,kupiga soga,ulevi muda wa kazi.
- Ukishatambua hapo juu kinachofuata ni kujua sababu zote zinazopelekea hali hiyo.Hapa unaweza kufanya maamuzi magumu na ya msingi kwa mfano kuepuka marafiki wenye msongo mbovu(unaokupelekea kukosa nidhamu kibiashara).
USHAURI
Unapokuwa na malengo fulani ni vema ukatafuta walau watu ambao unaona watakuwa msaada kwako kufikia utakapo. Mara nyingine unaweza ona kuwa unaweza kustahimili wewe mwenyewe bila msaada mwingine.Lakini unapochukua ushauri inaweza kukurahisishia muda wa kutatua tatizo.Maana kama ungalikuwa pekeako utawaza njia tofautitofauti(ambapo kuziwaza tu inakuchukua muda) pia utahitaji muda wa kuchagua wazo lililo bora kati ya uliyonayo.
Lakini kama ungekuwa umepata ushauri unakuwa na uwanja mpana wa kuchagua ndani ya muda mfupi kuliko kuwa peke ako.
Unapotaka kuingia kwenye biashara zingatia kipengele hiki kwa kufanya yafuatayo:
-Tafuta rafiki au ndugu anaekujua vizuri kuwa mshauri wako
-Huyu mtu anatakiwa kuwa yule unayemuamini na ni mjasiriamali pia mtenda kazi(anajibidisha katika biashara yake)
-Mtumie huyo katika kujua uwezo wako,wazo lako na changamoto unazoziona
-kesho mtafute huyo mshauri na umuorodheshee nlivoivovitaja hapo juu.
-Huu uwe mwongozo wako kwa wazo lako jipya
Chapisha Maoni