Imeandaliwa na
Charles Stephen Asande
Leo nataka tujifunze kuhusu mteja.Hapa tutapata kujua mambo tofauti tofauti yamhusuyo mteja.
Makampuni yaliyoendelea yana fokasi kwa mteja,Yanajipanga kufikia mahitaji ya wateja.
Mteja ni nani?
-Mteja ni mtu anayehitaji huduma/bidhaa/msaada kutoka kwako
-Mteja ni sababu ya wewe kuwa hapo ulipo.
-Mawasiliano baina ya mtoa huduma na mteja
Huduma nzuri kwa mteja ni ile ya kummsaidia mteja zaidi ya kile anachouliza.
MBINU BORA KUMVUTA WATEJA
-Vaa vizuri
-Furahia kusaidia watu
-Wahudumie vizuri
-Wajali wateja wako
-Wahudumie kwa usawa
-Tambua watu wenye mahitaji ya pekee
-Kuwa msafi
-Jiamini
-Kuwa na mpangilio mzuri
WATEJA WENYE MAHITAJI YA KIPEKEE
-Wateja wanaozungumza lugha tofauti
-Watu wenye ulemavu
-Wageni wa mji au maeneo ulipo
-Watoto
JINSI YA KUMHUDUMIA WATEJA
-Kuwa shapu,msalimu na kumkaribisha mteja mara moja unapomuona hata kama upo bize
-Tabasamu
-Usitumie lugha ya ukali
-Mwache awe huru
-Muulize anachohitaji usihisi ni nini anaweza hitaji
-Mfanye ajione ni muhimu kwako na unamthamini
-
-Msikilize kwa umakini
-Tambua tamaduni za watu wa mazingira(ili uweze wasalimia na kuwakaribisha ipasavyo)
-Mtambulishe aina,ubora wa bidhaa na huduma yako.
-Maliza kwa kuwashukuru na kumkaribisha tena
-Waelimishe wateja wako.
Kumbuka:-Huduma kwa mteja inaisha pale anaporidhika.
-Wewe sio mteja! hivo sio kila unachokiona ni ubora katika bidhaa na mteja atakiona hivohivo(msikilize )
MAMBO YA KUEPUKA KUFANYA KWA MTEJA
-Kumwambia Sijui bila kumpa mbadala
-Kutokumjali mteja kwa kuwa upo bize
-Kuwahudumia kwa utofauti(kujali baadhi na kutojali wengine)
-Kumtolea lugha chafu
like our facebook page Vijana Tunaweza Kujiajiri
Chapisha Maoni