Unknown
Charles Stephen Asande
Are you an African ground breaker? Can you innovate for positive change? Do you want to be part of the growing innovation movement in Africa? Does your innovation boast the ‘Made I Africa’ brand? Enter the 2016 Innovation Prize for Africa (IPA). The IPA honours and encourages innovative achievements that contribute toward developing new products, increasing efficiency or saving cost in Africa. The prize also promotes also among young African men and women the pursuit of science, technology and engineering careers as well as business opportunities with potential of contributing to sustainable development in Africa.
IPA Priority Areas
  • Agriculture and agricbusiness
  • Environment
  • Energy and water
  • Health and well-being
  • ICTs
  • Manufacturing and service industry
WORTH
  • 1st Prize (the overall winner whose innovation demonstrates the best innovation with clear business potentials): $100,000 USD
  • 2nd Prize (The innovator who best demonstrates a commercially-driven business innovation): $25,000 USD
  • Special Prize for Social Impact (the innovation that demonstrates the greatest social impact): $25,000 USD
  • Nominees: the top 10 nominees shall be invites for face-to-face interviews to assess in depth their innovation as potential winners for the IPA competition.
  • AIF will provide a $5,000 USD voucher to each nominee to assist in moving the innovation to the next step.
ELIGIBILITY
  • Innovations must be by Africans for Africa
  • Africans in Diaspora can also enter if their innovations are significant to Africa
DEADLINE: October 31, 2015
To apply and for more information visit here
Unknown



 Imeandaliwa na
 Charles Stephen Asande
Leo nataka tujifunze kuhusu mteja.Hapa tutapata kujua mambo tofauti tofauti yamhusuyo mteja.
 Makampuni yaliyoendelea yana fokasi kwa mteja,Yanajipanga kufikia mahitaji ya wateja.

Mteja ni nani?
    -Mteja ni mtu anayehitaji huduma/bidhaa/msaada kutoka kwako
-Mteja ni sababu ya wewe kuwa hapo ulipo.


-Mawasiliano baina ya mtoa huduma na mteja
Huduma nzuri kwa mteja ni ile ya kummsaidia mteja zaidi ya kile anachouliza.

MBINU BORA KUMVUTA WATEJA

-Vaa vizuri
-Furahia kusaidia watu
-Wahudumie vizuri
-Wajali wateja wako
-Wahudumie kwa usawa
-Tambua watu wenye mahitaji ya pekee
-Kuwa msafi
-Jiamini
-Kuwa na mpangilio mzuri

WATEJA WENYE MAHITAJI YA KIPEKEE

-Wateja wanaozungumza lugha tofauti
-Watu wenye ulemavu
-Wageni wa mji au maeneo ulipo
-Watoto

JINSI YA KUMHUDUMIA WATEJA

-Kuwa shapu,msalimu na kumkaribisha mteja mara moja unapomuona hata kama upo bize
-Tabasamu
-Usitumie lugha ya ukali
-Mwache awe huru
-Muulize anachohitaji usihisi ni nini anaweza hitaji
-Mfanye ajione ni muhimu kwako na unamthamini
-
-Msikilize kwa umakini
-Tambua tamaduni za watu wa mazingira(ili uweze wasalimia na kuwakaribisha ipasavyo)
-Mtambulishe aina,ubora wa bidhaa na huduma yako.
-Maliza kwa kuwashukuru na kumkaribisha tena
-Waelimishe  wateja wako.
Kumbuka:-Huduma kwa mteja inaisha pale anaporidhika.
        -Wewe sio mteja! hivo sio kila unachokiona ni ubora katika bidhaa na mteja atakiona hivohivo(msikilize )

MAMBO YA KUEPUKA KUFANYA KWA MTEJA

-Kumwambia Sijui bila kumpa mbadala
-Kutokumjali mteja kwa kuwa upo bize
-Kuwahudumia kwa utofauti(kujali baadhi na kutojali wengine)
-Kumtolea lugha chafu



like our facebook page  Vijana Tunaweza Kujiajiri



Unknown
                                                                 






Imeandaliwa   na                                                                                                                                       Charles Stephen Asande 

   1.Mtu anawezaje kufanikiwa kupitia ujasiliamali?
 Uchunguzi unaonesha kuwa wajasiliamali wenye maendeleo wana tabia fulani zinazofanana.Uchunguzi huu hautabiri mafanikio kwako,Ila unaweza kukupa msingi mzuri katika kuanza biashara kwa kukufanya
uwe mwangalifu katika kujua kipi ni bora au muhimu kukijua kiundani kabla hujaingia kwenye biashara.

Unapima vipi uwezo wako katika kufanikiwa?.Jiulize maswali yafuatayo
-Je ninaweza kuvumilia nitapokutana na magumu?
-Je nina nia ya dhati kujiongoza mwenyewe?
-Je maamuzi ninayofanya yatafanya mabadiliko ya kweli?
-Je nina uwezo wa kuona kila kona ihusuyo biashara?
-Je nina msukumo utaoniwezesha kufanya kazi kwa bidii?
-Je nina uelewa wowote wa biashara yoyote?

Haimaanishi kila mfanyabiashara mwenye maendeleo alikuwa na majibu ya "NDIYO" kwa maswali hayo juu.Yawezekana ukawa na "HAPANA" kwa baadhi ya maswali.Usivunjike moyo tafuta msaada na ushauri utakaokusaidia kufika malengo yako!.

2.Ninatambua vipi kama ninaweza kuanza biashara?
 Biashara ndogondogo zina vitu vingi vinavyofananafanana.Yafuatayo ni sifa za kukuwezesha kufanikiwa katika biashara.
-Kuwa tayari kujitoa
  Ujasiliamali unshitaji kujitoa katika muda,hali na maamuzi pia.
-Uchangamfu
-Utahitajika kuwachangamkia watu tofautitofauti kwa mfano wateja,wafanyakazi(uliowaajiri au unaofanya nao kazi katika biashara  mfano wasafirishaji) na watu wa mauzo(wasambazaji) kama hupendi kuongea na watu usio wajua, biashara inaweza kuwa ngumu kwako.
-Uwezo wa kuongoza na kujiongoza
 Watu watahitaji majibu ya maswali yao(bidhaa/huduma).Hivo basi yakupasa kujua ni namna gani unajipanga katika kuhakikisha unawapa majibu yao kwa wakati.Wakati huohuo unaongeza idadi ya watu wenye maswali.
Jipime uwezo wako na jifunze kutoka kwa watu waliofanikiwa katika hiyo biashara.Je unaweza kuzidisha huduma na kupita wengine? Je unahitaji elimu gani ili kukidhi mahitaji ya wateja wako?

Pitia majarida,vipeperushi mbalimbali zinazohusu biashara ili upate kujifunza kutoka sehemu na watu tofautitofauti.
3. Ninawezaje kukuza soko langu?

 Kwanza yabidi kujua wateja wako ni akina nani.Pia inabidi ujue kiundani kuhusu soko lako!.
-Je soko lako ni lipi hasa?
-Wateja wako wanatoka wapi hasa?(mijini,vijijini,watalii n.k)
-Ni kwa nini wanunue kwako?(Vitu vya kuangalia ubora,bei,mazingira,huduma,promosheni)
-Vitu gani wateja wanaviangalia katika bidhaa?
Utafiti utakupa majibu ambayo yana zaidi ya uzoefu wako katika biashara!
4.Je kuna mtu yeyote anaweza kuwa na majibu kwa maswali yangu?

  Hapa yakubidi utambuwe uwezo wa watu tofautitofauti walio kwenye biashara na washauri wa kibiashara kupitia semina,radio,television n.k

5.Kwa nini nataka kuanza kufanya biashara?

6.Ni biashara gani nataka kuifanya?

7.Wateja wangu ni akina nani?

8.Huduma/bidhaa gani biashara yangu itatoa!?

9.Je nipo tayari kutumia muda na hela ili kuanzisha biashara?


10.Ni tofauti gani nitaiweka katika biashara tofauti na wengine?

11.Biashara yangu nitaifanyia wapi?

12.Je ninahitaji kuajiri mtu/watu?(wangapi?)

13.Bidhaa zangu nitazipata wapi/kwa nani?

14.Kiasi gani cha pesa nitakihitaji?

15.Je nitahitaji mkopo?

16.Ni muda gani itanichukua mpaka bidhaa/huduma kuwaa sokoni?
17.Ni muda gani utanichukua mpaka kuanza kupata faida?
18.Nani ni washindani zangu?
19.Niuzaje bidhaa zangu?
20.Biashara hiyo ni halali?(Au ninawezaje kufanya taratibu za kisheria kwa hiyo biashara?)
21.Kodi zipi ninapaswa kulipa kwa biashara yangu?
22.Aina zipi za Bima nazihitaji katika biashara yangu?
23.Namna gani nitaisimamia Biashara yangu?
24.Nitatangaza vipi biashara yangu?

Unknown
                                                 



Imeandaliwa na;
 Charles Stephen Asande:

MJASILIAMALI
-Ni mtu anayetafuta fursa yenye manufaa na kuamua kuiweka katika biashara.


SABABU TOFAUTI ZINAZOWAPELEKA WATU KATIKA UJUASILIAMALI
-Kuchoshwa na Kazi za kuajiriwa

 Hapa ni mahali mtu anaweza kupanga ratiba(biashara) zake bila kuingiliwa na nguvu yeyote(Shinikizo).


-Hitaji la kutatua mactatizo ya watu(kibiashara)


Uwepo wa matatizo katika jamii ndio unaopelekea wajasiliamali kuwepo.Hapa wao huona kwanza tatizo kisha hulitatua kwa njia zitazowainua wao wakati huohuo zikitatua tatiza husika katika jamii.

-Hitaji la kufanikiwa kimaisha

 Wajasiliamali ni watu wanaojenga/kuimarisha uchumi hivo kupelekea maisha yao pia kuwa ya mafanikio.


-Kuondokana na tatizo la kukosa ajira



Kutokana na Mitikisiko ya kiuchumi makampuni mengi tena makubwa yamekuwa yakipunguza wafanyakazi kuliko wanaowaajiri.Hivyo iwe kwa msomi au mtu mwingine wa kawaida ni lazima kulifikiria hili jambo kwa umakini.Hapa ndipo watu huona njia inayowapelekea katika ujasiliamali.



-Hamu ya kutaka kuishi maisha uyapendayo


 Kuanza biashara kunakufanya kuwa huru kupanga lini,wapi na namna gani ufanye shughuli zako



-Tabia za watu wenye maendeleo
                                                    1.MAONO MAKINI

  Mjasiliamali huanza na wazo kuu  lenye kubeba jinsi/namna gani anaweza kulifanya WAZO LAKE KIBIASHARA(Bussiness Idea) lifanikiwe

2.KUJITUMA


 Mjasiliamali siku zote huwa tayari kufanya kazi tena kwa bidii ili kufikia malengo yake

3.UBUNIFU

  Mjasiliamali hubuni mbinu rahisi kukabiliana na  matatizo/hali ngumu kwa jamii/mazingira aliyopo

4.UTAYARI.

  Mjasiliamali hana hofu katika gumu lolote analokutana nalo, Zaidizaidi yeye hujipanga vema na kuendelea mbele

5.UVUMILIVU

   Katika kila unapopita kuna hali unaweza kutana nazo ambazo zinakuhitaji kuwa mvumilivu.Vivohivo kwa mjasiliamali kuna wakati unaweza ona hakuna dalili ya mafanikio kwa wakati ujao lakini usikate tamaa jibidishe zaidi na zaidi.Siku zote hakuna njia ambayo ni mteremko moja kwa moja.

 6.NIDHAMU


Katika Maendeleo hiki kipengele ni muhimu.Unaweza ukawa na biashara nzuri lakini ukiwa na nidhamu mbovu unaweza kuta unapiga marktime(hauendelei).Kama mjasiliamali yapasa kuwa na nidhamu kwa biashara yako(wateja wako) na matumizi yako(Nidhamu ya pesa).
   Ili kutunza nidhamu fanya yafuatayo:
-Ujue vitu vyote vinavyoshusha nidhamu katika nyanja zako zote kibiashara(n.b biashara na matumizi) Kwa mfano kuchat,kucheza bao,drafti,kupiga soga,ulevi muda wa kazi.
- Ukishatambua hapo juu kinachofuata ni kujua sababu zote zinazopelekea hali hiyo.Hapa unaweza kufanya maamuzi magumu na ya msingi kwa mfano kuepuka marafiki wenye msongo mbovu(unaokupelekea kukosa nidhamu kibiashara).




                                                                    USHAURI



Unapokuwa na malengo fulani ni vema ukatafuta walau watu ambao unaona watakuwa msaada kwako kufikia utakapo. Mara nyingine unaweza ona kuwa unaweza kustahimili wewe mwenyewe bila msaada mwingine.Lakini unapochukua ushauri inaweza kukurahisishia muda wa kutatua tatizo.Maana kama ungalikuwa pekeako utawaza njia tofautitofauti(ambapo kuziwaza tu inakuchukua muda) pia utahitaji muda wa kuchagua wazo lililo bora kati ya uliyonayo.
Lakini kama ungekuwa umepata ushauri unakuwa na uwanja mpana wa kuchagua ndani ya muda mfupi kuliko kuwa peke ako.

Unapotaka kuingia kwenye biashara zingatia kipengele hiki kwa kufanya yafuatayo:

-Tafuta rafiki au ndugu anaekujua vizuri kuwa mshauri wako
-Huyu mtu anatakiwa kuwa yule unayemuamini na ni mjasiriamali pia mtenda kazi(anajibidisha katika biashara yake)
-Mtumie huyo katika kujua uwezo wako,wazo lako na changamoto unazoziona
-kesho mtafute huyo mshauri na umuorodheshee nlivoivovitaja hapo juu.
-Huu uwe mwongozo wako kwa wazo lako jipya


 
Unknown
By Hamad
Soko letu limekuwa
likiwanufaisha zaidi wageni
na wananchi wa nchi jirani
ambao hulitumia kikamilifu
kujinufaisha na wazalendo
wengi kutoelewa nini
kinachoendelea. Kwa wale
waliokwisha jitosa, huwezi
amaini jinsi wanavonufaika
na kuwekeza zaidi na zaidi.
Leo kidogo tutupe jicho kwenye hii sekta ya
hisa… Si sekta ngeni sana ila kwa hapa
nchini wananchi wengi hawajaigundua na
kushiriki kikamilifu kama nchi jirani na
Tanzania. Wenzetu Kenya wamejitahidi
kwenye ushiriki wa soko lao la Hisa la
Nairobi (Nairobi Stock Exchange). Na kwa
Afrika Mashariki, hili Soko la Hisa la Nairobi
ndilo soko kubwa kuliko yote.
Soko letu la hisa la Dar es Salaam (DSE)
japo kila siku limekumbatia usemi ni soko
geni nchini, lina zaidi ya miaka  15 tangu
lianze kufanya biashara mwaka 1998 mwezi
wa Aprili. Kwa muda wote huu wa miaka 15
soko limekuwa halina ukuaji  wa kuridhisha
wala kuvutia. Mpaka leo 2013 kampuni
zilizojisajili ni 17 tu, (Soma hapa zaidi http://
www.dse.co.tz/main/index.php?page=5)
Idadi ya wananci wanaoshiriki kuuza na
kununua hisa bado ni ndogo sana na uelewa
wa jamii juu ya hili soko ni mdogo sana!
Pamoja na changamoto zake, hili soko lina
faida kubwa kwa wale walioligundua na
wanaoendelea kulitumia. Kuna mjasiriamali
mmoja, yeye alinunua hisa za Twiga
mwishoni mwa miaka ya 90 au mwanzoni
mwa miaka ya 2000 zikiwa zinauzwa kati ya
200-300 kwa kipande. Leo hii kipande hicho
hicho cha Twiga Cement kinauzwa kati ya
2500-2006 kiasi cha miaka 13 tu mbele.
Mdau huyu wa soko hilo anakiri kama
angejua ukuaji ni wa kiasi hiki basi
angenunua zaidi ya hizo alizonunuaga. Na
ameendelea kuongeza vipande vyake kila
awezapo. Anadai yeye hupenda kuwekeza
kwenye hisa sababu hakuna usumbufu wa
uendeshaji . Ukishanunua hisa unakaa na
kungoja zipande ama zishuke ili na wewe
uuze za kwako. Anakiri kuwa soko hili
limemnufaisha sana na anawashauri wengine
wajiunge nalo wapate kunufaika pia.
Wengi wetu wenye mitaji midogo midogo
tunaweza kunufaika kwa kujiunga na hili
soko la hisa la Dar es Salaam na kununua
vipande kwa pesa tuliyonayo. Vipande vingi
vimeonesha kupanda thamani yake ikiwemo
hisa za makampuni ya bia (TBL na SBL),
Saruji (Twiga  na Simba ) na Bank kama
NMB. Kama mwekezaji mzalendo, ukijitosa
ukanunua hisa zako za 2,000,000 leo, baada
ya miaka 4 unaweza kuziuza hata kwa faida
kubwa tu bila kuteseka na usumbufu wa
uendeshaji kama zilivyo biashara nyingine.