Unknown
By Hamad
Soko letu limekuwa
likiwanufaisha zaidi wageni
na wananchi wa nchi jirani
ambao hulitumia kikamilifu
kujinufaisha na wazalendo
wengi kutoelewa nini
kinachoendelea. Kwa wale
waliokwisha jitosa, huwezi
amaini jinsi wanavonufaika
na kuwekeza zaidi na zaidi.
Leo kidogo tutupe jicho kwenye hii sekta ya
hisa… Si sekta ngeni sana ila kwa hapa
nchini wananchi wengi hawajaigundua na
kushiriki kikamilifu kama nchi jirani na
Tanzania. Wenzetu Kenya wamejitahidi
kwenye ushiriki wa soko lao la Hisa la
Nairobi (Nairobi Stock Exchange). Na kwa
Afrika Mashariki, hili Soko la Hisa la Nairobi
ndilo soko kubwa kuliko yote.
Soko letu la hisa la Dar es Salaam (DSE)
japo kila siku limekumbatia usemi ni soko
geni nchini, lina zaidi ya miaka  15 tangu
lianze kufanya biashara mwaka 1998 mwezi
wa Aprili. Kwa muda wote huu wa miaka 15
soko limekuwa halina ukuaji  wa kuridhisha
wala kuvutia. Mpaka leo 2013 kampuni
zilizojisajili ni 17 tu, (Soma hapa zaidi http://
www.dse.co.tz/main/index.php?page=5)
Idadi ya wananci wanaoshiriki kuuza na
kununua hisa bado ni ndogo sana na uelewa
wa jamii juu ya hili soko ni mdogo sana!
Pamoja na changamoto zake, hili soko lina
faida kubwa kwa wale walioligundua na
wanaoendelea kulitumia. Kuna mjasiriamali
mmoja, yeye alinunua hisa za Twiga
mwishoni mwa miaka ya 90 au mwanzoni
mwa miaka ya 2000 zikiwa zinauzwa kati ya
200-300 kwa kipande. Leo hii kipande hicho
hicho cha Twiga Cement kinauzwa kati ya
2500-2006 kiasi cha miaka 13 tu mbele.
Mdau huyu wa soko hilo anakiri kama
angejua ukuaji ni wa kiasi hiki basi
angenunua zaidi ya hizo alizonunuaga. Na
ameendelea kuongeza vipande vyake kila
awezapo. Anadai yeye hupenda kuwekeza
kwenye hisa sababu hakuna usumbufu wa
uendeshaji . Ukishanunua hisa unakaa na
kungoja zipande ama zishuke ili na wewe
uuze za kwako. Anakiri kuwa soko hili
limemnufaisha sana na anawashauri wengine
wajiunge nalo wapate kunufaika pia.
Wengi wetu wenye mitaji midogo midogo
tunaweza kunufaika kwa kujiunga na hili
soko la hisa la Dar es Salaam na kununua
vipande kwa pesa tuliyonayo. Vipande vingi
vimeonesha kupanda thamani yake ikiwemo
hisa za makampuni ya bia (TBL na SBL),
Saruji (Twiga  na Simba ) na Bank kama
NMB. Kama mwekezaji mzalendo, ukijitosa
ukanunua hisa zako za 2,000,000 leo, baada
ya miaka 4 unaweza kuziuza hata kwa faida
kubwa tu bila kuteseka na usumbufu wa
uendeshaji kama zilivyo biashara nyingine.